KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, November 11, 2010

BBC yafichua njama za Jemedari wa DRCBBC imefichua ushahidi Jemedari mmoja wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alitumia nguvu za kijeshi kusaidia kampuni moja kuchukuwa udhibiti wa mgodi mmoja wa dhahabu a baadae kupatiwa mgao wa dhahabu kutoka mgodi huo.Mwandishi wa BBC aligundua kuwa Jemedari Amisi Kumba aliamuru kutimuliwa kwa kampuni moja katika mgodi wa dhahabu wa Omate mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na badala yake kutoa mgodi huo kwa kampuni moja ijulikanayo kama Geminaco.

Kuna ushahidi unaonyesha Jenerali Kumba alifanya makubaliano na kampuni ya Geminaco kupata mgao wa asilima 25 ya dhahabu kutoka mgodi huo.

Mkuu wa kampuni ya Geminaco amekanusha madai hayo na kukataa kujibu maswali kuhusiana na swala hilo

No comments:

Post a Comment