KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 3, 2010

MR II aka 'Sugu' Sasa Awa Mheshimiwa, Awa Mbunge wa Mbeya Mjini



Msanii mkongwe wa Bongo Flava MR II aka "Sugu" amekuwa mbunge wa Mbeya Mjini



Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi aka MR II au maarufu kwa jina la Sugu ameshinda uchaguzi wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA kwa kumbwaga vibaya mgombea wa CCM na wagombea wengine.
Joseph Mbilinyi aka MR II amepanda chati na sasa atakuwa akijulikana kama Mheshimiwa Joseph Mbilinyi baada ya kufanikiwa kuingia kwenye bunge la kutunga sheria la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MR II alishinda uchaguzi wa Mbeya Mjini kwa kuwabwaga vibaya wapinzani wake, Benson Mpesya wa CCM, Prince Mwaihojo, wa CUF, Tokolasi Kasuluari wa DP na Aggabo Mwakatobe wa NCCR.

Msimamizi wa jimbo hilo alimtangaza MR II kuwa ni mshindi wa jimbo hilo baada ya kupata kura 46,411 huku mpinzani wake mkubwa toka CCM, Benson Mpesya akifuatia kwa mbali akiwa na kura 24,327.

MR II anatarajiwa kuwa mtetezi mkubwa wa maendeleo ya jimbo lake na wasanii wa muziki wa Bongo Flava nchini.

Wakati wa kampeni, kundi la muziki wa kizazi kipya la Wagosi wa Kaya kutoka Tanga, lilitoka na kitu kipya kiitwacho ‘Sugu Nenda Bungeni’, kikiwa ni maalum kwa ajili ya kumpigia debe aingie Bungeni.

Wakiongea na Nifahamishe.Com wakati wa kampeni, Wagosi wa Kaya walisema kuwa Walisema kuwa wanamfahamu vilivyo Sugu kwa jinsi alivyo mpigania haki na mtetezi wa wanyonge hivyo wanaamini akiwa bungeni atakuwa na nafasi kubwa ya kuwatetea wananchi wa Mbeya na wasanii wa muziki nchini

No comments:

Post a Comment