KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, November 11, 2010

Mama Amuua Mwanae Baada ya Kumfua Kwenye Mashine ya Kufulia Nguo


Mtoto mchanga wa siku 10 amepoteza maisha yake baada ya mama yake kujisahau na kumchanganya pamoja na nguo na kumfua kwenye mashine ya kufulia nguo kwa dakika 40.
Polisi wa Bartlesville, Oklahoma nchini Marekani wanamshikilia mama aliyemuua mwanae kwa bahati mbaya kwa kumchanganya na nguo chafu alizozifua kwenye mashine ya kufulia nguo.

Lindsey Fiddler, amefunguliwa mashtaka ya mauaji huku akitupwa rumande akinyimwa dhamana kwa kosa la mauaji ya mwanae yaliyotokea alhamisi iliyopita.

Shangazi wa mtoto aliyefariki aliita ambulansi na polisi punde baada ya kumgundua mtoto huyo mchanga akiwa ndani ya mashine ya kufulia nguo.

Shangazi huyo aliwaambia polisi kuwa alifika nyumbani kwa Lindsey kuwaona watoto wake, wakati huo Lindsey alikuwa amelala fofofo.

Aliwaambia polisi kuwa alipata tabu kumuasha Lindsey ambaye wakati huo alikuwa kwenye usingizi mzito kutokana kulewa pombe na madawa ya kulevya.

Madaktari walijaribu kuyaokoa maisha ya mtoto huyo wakati wakimwahisha hospitali kwa ambulansi lakini hawakufanikiwa.

Mtoto huyo mchanga alifariki dunia kutokana na kuzungushwa ndani ya mashine ya kufulia nguo kwa takribani dakika 40.

Polisi wa Bartlesville walisema kwamba Lindsey alishawahi kukamatwa na kuhukumiwa kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya

No comments:

Post a Comment