KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Acheni kutoa picha zisizofaa za Rais-Uganda



Rais wa Uganda
Mkuu wa idara ya habari ya rais wa uganda Yoweri Museveni amesema kuwa sifa ya rais huyo imeharibiwa vibaya kutokana na mziki wa Rap aliouimba mwezi uliopita.

Tamale Mirundi amesema walaghai wameharibu picha za bwana Museveni, wakitumia komputa, na kumfananisha na nyota wa miziki ya Hip Hop anayeimba akiwa nusu uchi.


Baadhi ya picha hizo zinaonyesha amevalia mkufu shingoni huku akiwa na picha alizochorwa mwilini maarufu kama ''tattoos''.

Rais Museveni anawania muhula mwingine kama rais wa Uganda kutipia chama cha National Resistance Movement NRM

No comments:

Post a Comment