KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, November 11, 2010

Umoja wa Mataifa wafunga misaada Haiti

Machafuko Haiti

Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Haiti limefunga miradi yake ya kutoa msaada na kusema hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu ya maandamano yaliofanyika wakishutumiwa kueneza maradhi ya kipindupindu nchini humo.




Zaidi ya watu elfu moja wamefariki dunia baada ya kuibuka maradhi hayo.

Waandamanaji hao wanasema maradhi ya kipindupindu yalipelekwa nchini humo na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Nepal na kuenezwa kupitia kwa majitaka.

Hata hivyo Umoja wa Mataifa umesema majaribio yake ya kimatibabu hayajathibitisha madai hayo.

Kuna pia taarifa kwamba maandamano hayo yanachochewa na sababu za kisiasa na kihistoria.

Umoja wa Mataifa una kikosi cha kuimarisha usalama nchini Haiti ambacho kinaisaidia serikali.

Kikosi hicho kilikuwepo Haiti hata kabla ya kuripuka kwa maradhi ya kipindupindu na mtetemeko wa ardhi ambao uliharibu kabisa maeneo mengi ya mji mkuu wa nchi hiyo mwezi wa Januari.

No comments:

Post a Comment