KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 5, 2010

Zaidi ya 2500 kutofanya mitihani leo



WANAFUNZI wapatao 2863 hawataweza kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya kidato cha nne kwa kufutiwa usajili kutokana na kutokuwa na sifa sahihi.
Wanafunzi hao wakujitegemea wapatao 1376 na1487 wa mashuleni.

Wamefutiwa usajili huo na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na kutolewa taarifa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk. Joyce Ndalichako.

Ndalichako alieleza kuwa, jumla ya watahiniwa 1,135 wa kujitegemea wamebainika kuwa na matokeo ya kidato cha pili ambayo si sahihi.

Amesema watahiniwa hao wamewasilisha namba za mtihani za watu wengine na namba nyingine hazipo kwenye matokeo ya kidato cha pili kwa mwaka husika.

Amesema na wengine walibainika kughushi huku wengine wamebainika kufanya mtihani yao ya kidato cha pili mwaka jana hivyo hawastahili na hawana sifa za kufanya mtihihani hiyo kwa mwaka huu

No comments:

Post a Comment