KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 2, 2010

Baba Ambaka Binti Yake Mara 360 Atupwa Jela Miaka 14,400
Baba wa nchini Philippines ambaye alimbaka binti yake mwenye umri wa miaka 13 karibia kila siku kwa muda wa mwaka mmoja, amehukumiwa kwenda jela miaka 14,400.
Mahakama ya nchini Philippines imemhukumu kwenda jela miaka 14,400 baba aliyembaka binti yake mwenye umri wa miaka 13 mara 360 ndani ya mwaka mmoja.

Baba huyo awali alihukumiwa adhabu ya kifo mwaka 2006 kwa makosa hayo ya ubakaji ambayo aliyafanya wakati mama wa mtoto huyo alipokuwa nje ya nchi kikazi.

Ikitoa hukumu ya kesi hiyo ijumaa iliyopita, mahakama ya rufaa ya mjini Manila ilitengua adhabu ya kifo aliyohukumiwa baba huyo na badala yake ilimhukumu kwenda jela miaka 40 kwa kila kosa moja la ubakaji alilofanya baba huyo.

Kwa makosa yake 360 ya ubakaji yaliyokuwa yakimkabili baba huyo alijikuta akihukumiwa kwenda jela jumla ya miaka 14,400.

Binti aliyebakwa na baba yake ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 22, aliiambia mahakama kuwa baba yake alianza kumbaka mwezi januari mwaka 2001 baada ya mama yake kusafiri kwenda Hong Kong kufanya kazi za ndani na kumuacha yeye pamoja na ndugu zake wawili pamoja na baba yao kwenye kitongoji cha Los Banos, kusini mwa Manila.

Mkasa huo wa ubakaji uligundulika mwaka mmoja baadae baada ya binti huyo kwenda kuwatembelea ndugu wa mama yake na kugoma kurudi kwa baba yake.

Huku akilia binti huyo aliwaelezea ndugu wa mama yake jinsi baba yake alivyokuwa akimbaka karibia kila siku. Mama yake alirudi toka Hong Kong na kumfungulia kesi mahakamani mumewe.

Mahakama ilitupilia mbali utetezi wa baba huyo kuwa alizushiwa kesi hiyo na mkewe ili aweze kuwachukua watoto akaolewe na mwanaume mwingine nje ya nchi.

Haijajulikana kama baba huyo atakata rufaa hukumu hiyo ya kwenda jela miaka 14,400

No comments:

Post a Comment