KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, October 5, 2010

Kortini kwa kulazimisha anyonywe nyetiJOHN Anthony [29] mkazi wa Kigogo jijini Dar es Salaam, anasota rumande kwa kukosa dhamana baada ya kufikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na shitaka la kumlazimisha mtoto wa miaka 14 amnyonye sehemu zake za siri.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa kujibu shitaka hilo mwishoni mwa wiki katika mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni mbele ya Hakimu Flora Mtarania na upande wa Mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Nassoro Sisiwaya.

Sisiwaya alidai mahakamani hapo kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 23, mwaka huu huko katika eneo la Kigogo anapoishi mshitakiwa huyo.

Sisiwa aliendelea kudai kuwa, siku ya tukio mshitakiwa alimlazimisha mtoto huyo wa kike mwenye umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) amnyonye sehemu zake za siri kwa manufaa yake binafsi.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, tendo hilo ni ukiukwaji wa sheria na kuvunja maadili ya watoto.

Hakimu alipomtaka mshitakiwa huyo kujibu shitaka hilo alikana, kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 13, mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa tena

No comments:

Post a Comment