KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 13, 2010

'Wezi wa simu' wauawa Afrika Kusini




Ramani ya Afrika Kusini


Watu sita wanakabiliwa na makosa ya mauaji baada ya kudaiwa kuwapiga mawe na kuua watu wawili wanaodaiwa kuiba simu ya mkononi Afrika Kusini.

Polisi walisema, kundi hilo, wakiwemo wanawake watatu, wanadaiwa kuwaua watu hao siku ya Jumapili jioni, katika jimbo la Limpopo.

Polisi hao imewasihi watu wasichukue sheria mikononi mwao wenyewe.

Waandishi wanasema makundi ya watu aghlabu huwapiga na kuua wanaoshukiwa kuwa wezi Afrika Kusini, ambao wengi wamekosa imani na mfumo wa sheria.

Msemaji wa polisi wa Limpopo Lt-Col Mohale Ramatseba alisema katika taarifa yake, " Kuchukua sheria mikononi inapingwa vikali".

"Mtu yeyote anayeshukiwa kuhusishwa katika uhalifu aripotiwe polisi ili wafikishwe mahakamani."

Alisema madai ya wizi huo wa simu haukuripotiwa polisi.

Hatua ya kuchukua sheria mkononi ni jambo la kawaida Afrika Kusini, ambapo kuna wasiwasi mkubwa katika vitongoji hasa juu ya nyumba duni, huduma na uhalifu.

Miaka miwili iliyopita, kulikuwa na mashambulio ya kutisha dhidi ya raia wa kigeni, waliokuwa wakilaumiwa kwa kuwaibia kazi wenyeji na kuongezeka kwa uhalifu.

Kundi hilo litafikishwa mahakamani Oktoba 20

No comments:

Post a Comment