KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 2, 2010

Wenye ulemavu wa macho warahisishiwa ilani za uchaguziMTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umezindua ilani maalum kwa watu wenye ulemavu wa macho kwa kutoa ilani hizo kwa maandishi maalum ya nukta itakayowaongoza kutambua na kuelewa ilani za vyama katika uchaguzi

Ilani hiyo imezindulia jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Maendeleo ya Walemavu (ADDI), Bw. Sixbert Mbaya.

Mbaya alisema kuwa, ilani hiyo itawawezesha wasioona kutumia haki yao ya msingi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu ujao wa Oktoba 31 mwaka huu kwa kuwa wataweza kuisoma na kutafakari

Alisema pia ilani hiyo wataweza kushiriki kikamilifu na kuzijua sera za wagombea na kuweza kuwahoji wagombea hao wanaoomba ridhaa ya kuchaguliwa.

Hivyo ilani hiyo imefanya kila mtanzania kushiriki vyema katika uchaguzi mkuu ujao na kutoacha nyuma watu wa jaamii hiyo ya walemavu kwani awali waliona kama wamebaguliuwa

No comments:

Post a Comment