KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 2, 2010

Indonesia: Ajali ya treni yawaua 30
Ajali ya treni Indonesia


Treni moja ya safari za usiku imegongana na nyingine iliyosimama katika kituo cha reli katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta karibu na mji wa Petarukan , kaskazini mwa Java.

Maafisa wa afya wanasema kuwa watu thelathini wamefariki japo inahofiwa kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Wengine wengi wamejeruhiwa na wamenaswa katika mabaki ya treni hiyo iliyong'oka kutoka reli na kubingiria mara kadhaa.

Uchunguzi umeanzishwa juu ya kilichosababisha ajali hiyo, ukiwemo uwezekano kuwa dereva wa treni hiyo huenda alivuka alama ya kusimama, au iwapo taa za barabarani hazikuwa zinafanya kazi vyema.

No comments:

Post a Comment