KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 2, 2010

Wanafunzi waunguza bweni baada ya kuzuiliwa kufanya mitihaniWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Ntunduru mkoani Mwanza wamechoma bweni moto baada ya kutangaziwa kuwa hawatashiriki kufanya mitihani yao ya mwisho inayotarajiwa kuanza Oktoba 4.
Shule hiyo iliyopo wilayani Sengerema imedaiwa kuwa tukio hilo la uchomaji bweni moto ulifanyika jana, majira ya jioni ya saa 1.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Nonosius Komba, alisema kuwa, wanafunzi hao walichukizwa na taarifa ya wakaguzi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwatangazia wanafunzi hao kuwa hawaatafanya mitihani hiyo kwa kuwa shule hiyo imekuwa haijasajiliwa.

Hivyo kutokana na matangazo hayo wanafunzo hao ambao wameonekana kughadhibika walichukua uamuzi huo kwa kuwa walidai kuwa walikuwa wakilipishwa ada mbalimbali kwa ajili ya mitihani hiyo na walishangazwa kusikia taarifa hiyo kutoka wizarani.

Hata hivyo Kamanda huyo alisema kuwa uchunguzi juu ya tukio hio unaendelea baada ya mahojiano maalum kufanyika na kuwasaka waneafunzi waliohusika katika tukio hilo

No comments:

Post a Comment