KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, October 14, 2010

Walinda usalama wawaua wafungwa Haiti



Makabiliano makali ya bunduki wameripotiwa kuendelea kwa saa kadhaa katika gereza kubwa zaidi nchini Haiti. Wafungwa katika gereza hilo waliokuwa wamepanga kutoroka walikuwa wamenyang'anya silaha walinzi na kufungua milango ya jela.

Kundi hilo la wafungwa linaarifiwa kuwachukua mateka walinzi watano, wahudumu wawili wa kutoa misaada na afisa mwingine wa gereza. Baadaye waliwaachilia wahudumu hao wawili.

Kwa kuhofia kwa wafungwa hao wangetoroka wasimamizi wa gereza hilo waliomba msaada kutoka kwa maafisa wa Umoja wa Mataifa. Magari kadhaa ya kivita na maafisa wa kuzima ghasia walitumwa katika gereza hilo.

Kwa mjibu wa Msemaji wa polisi Franz Lerebours watatu kati ya watekaji nyara hao waliuawa katika oparesheni hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa ghasia kutokea katika gereza hilo. Katika siku zilizopita wafungwa wamezusha vurugu wakipinga hali mbaya ya maisha.

Hali ya utulivu imeripotiwa kurejea na mateka wote wameachiliwa huru. Maafisa wa Umoja wa Mataifa bado wanashika doria.

Hata hivyo kuna hofu kuwa huenda kukawa na matatizo zaidi kwani magereza mengi yaliporomoka wakati wa tetemeko la ardhi mwezi Januari na maelfu ya wafungwa wangali mafichoni

No comments:

Post a Comment