KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, October 14, 2010

Somalia: Majeshi yatwaa mji kutoka kwa Al-Shabaab



Majeshi ya Serikali ya mpito ya Somalia yakisaidiwa na kundi la wapiganaji yamefaulu kuutwaa mji uliokuwa umetekwa na wanamgambo wa Al shabaab.

Mji huu wa Bulo Hawo, karibu na mpaka wa Kenya na Ethiopia umekuwa chini ya udhibiti wa kundi hili kwa mwaka mmoja.

Zaidi ya watu kumi wanaripotiwa kuuawa na wengine kumi na watano kujeruhiwa katika mapigano yaliyozuka kati ya makundi hayo mawili.

Walioshuhudia wameelezea kuzuka kwa hali ya wasiwasi katika eneo hilo na mamia ya wakaazi wametoroka makwao.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya mpito imearifu kuwa jeshi linaelekea katika miji mingine iliyo chini ya udhibiti wa kundi hilo kwa nia ya kuitwaa tena. Kundi la Al Shabaab hata hivyo halijatoa taarifa yoyote.

Kundi la Al-Shabaab linadhibiti maeneo kadhaa kusini mwa Somalia yanayopakana na eneo la kaskazini Mashariki mwa Kenya na limekuwa likiendesha kampeini ya kuiondoa mamlakani serikali ya mpito inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Hadi sasa maelfu ya watu wameuawa na maelfu wengine kuachwa bila makao katika mapigano kati ya wapiganaji hao wenye uhusiano wa karibu na kundi la kigaidi la Al-Qaeda kwa upande mmoja na majeshi ya serikali yanayoungwa mkono na majeshi ya muungano wa Afrika kwa upande mwingine.

No comments:

Post a Comment