KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, October 14, 2010

Nchi nne za Kiafrika kupambana na LRAJoseph Kony

Muungano wa Afrika umesema nchi nne zinaunda kikosi cha pamoja cha kupambana na kundi la waasi la Lord's Resistance Army.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Uganda ili kuzidisha shinikizo dhidi ya LRA ambalo ni kundi lililoundwa nchini Uganda miaka ishirini iliyopita.

Umoja wa Mataifa umesema kundi hilo limesababisha watu laki nne kukimbia makaazi yao katika miaka miwili iliyopita, na linashambulia miji na vijiji vilivyo mbali ya kilometer elfu moja kutoka makao yao ya asili.


Joseph Kony (alizaliwa mwaka 1961) ni kiongozi wa kundi la wanamugambo wa Lord's Resistance Army (LRA), kundi la kuvizia ambalolomejihusisha na kampeni za ghasia likiwa na azma ya kuanzisha serikali inyoongozwa na viongozi wa dini nchini Uganda, kundi hili liandai limejengeka kwenye misingi ya Biblia ya kikristo na amri kumi. [1] Kundi la LRA ambalo lilijulikana kwa vitendo vyake dhidi ya wenyeji wa Uganda Kaskazini, limeteka nyara takribani watoto 30,000 na kusababisha watu milioni 1.6 kukimbia makazi yao tangu uasi wao ulipoanza mwaka 1986.

WasifuJoseph Kony alizaliwa mwaka 1961 katika kijiji cha Odek, kinachopatikana mashariki mwa Gulu kaskazini mwa Uganda, wazazi wake walikuwa wakulima. Aliwapenda wadogo zake lakini walipomkosea aliwaadhibu. [5] Katika ujana wake, Joseph Kony alifunzwa kuwa mganga wa kijiji na kakake mkubwa, Benon Okello, na kakake alipoaga alichukua kikamilifu wajibu wa kuwa mganga wa kijiji. [6] Alipokosewa alipendela kupigana badala ya maelewano kwa njia ya mazungumzo. Akiwa shuleni alitaniwa kwa ukubwa wake na walimu walimpa wakati mgumu kwa sababu hakuonekana muerevu sana. Babake alikuwa mteandakazi wa mungu katika kanisa katoliki na mamake alikuwa Muangilikana, Kony alikuwa alatare kwa miaka kadhaa. Aliacha kwenda kanisani akiwa na umri wa karibu miaka 15. [5] Aliachaia masomo yake shule ya upili na alipata umaarufu mwezi wa Januari mwaka 1986, akiwa na miaka ishirini na kitu hivi. Kundi lake lilikuwa moja ya makundi makubwa yaliyoibuka huko Acholi wakati wa vuguvugu maarufu la Roho Mtakatifu lililoongozwa na Alice Auma (aka Lakwena). Hata hivyo kulikuwa na mgogoro miongoni mwa Wacholi walionung'unikia kupoteza uashawishi wao baada ya Rais Tito Okello aliyekuwa Muacholikupinduliwa na Yoweri Museveni na jeshi lake la National Resistance Army (NRA) wakati wa Vita vya msituni vya Uganda vilivyoisha mwaka 1986.

Mwanzoni, kundi la Kony's liliitwa United Holy Salvation Army (UHSA) na halikuchukiliwa kama tisho na NRA. Kufikia mwaka 1988, baada ya mkataba kati ya NRA na Uganda People's Democratic Army kuongeza makundi yake mengine ya wapiganaji pamoja na kusajili watoto kwa nguvu kulilifanya kundi la United Holy Salvation Army kuwa jeshi lililoogofya. Askarijeshi wake wengi walikuwa watoto. Inakadiriwa kuwa amechukuwa watoto zaidi ya 104.000 wavulana na wasichana tangu LRA ilipoanza kupigana mwaka 1986. MMara nyingi aliua jamaa na majirani wa watoto hawa alipokuwa akiwateka na kuwalazimisha wapigane katika jeshi lake. Kamanda wa kundi lilosalia la UPDA alikuwa Odong Latek, ambaye alifanikiwa katika kumshawishi Kony atumie mbinu za kisasa za kijeshi kinyume na majaribio ya awali ambayo yalihusu mashambulizi ya mslaba na kutumia maji matakatifu. Mbinu hii mpya ilifanikiwa na UHSA mapigano madgomadogo lakini waliweza kuwashinda NRA. Baada ya ushindi huu NRA ililipiza kizazi kwa kudhoofisha kundi la Kony kisiasa na kampeni iliyoitwa Oparation North.

Kufikia mwaka 1992 alilipa hilo kundi jiypa la Muungano wa Jeshi la Kikristo la Demokrasia na ni katika wakati huu ndiyo waliowateka nyara wasichana 44 kutoka shule za upili za Sacred Heart Secondary na St. Mary's Girls School Operation North iliharibu kabisa kile kingekuwa wanamugambo wa Lord's Resistance Army,hata hivyo, ingawa idadi yao ilipungua kutoka maelfu hadi mamia waliendelea kuwavamia raia na washirika wa NRA.

Mazungumzo ya Bigombe ya mwaka 1993 yalifunua mengi kumhusu Joseph Kony. Betty Bigombe alikumbuka kwamba mara ya kwanza alikutana na Kony na wafuasi wake walitumia mafuta kujikinga na risasi na pepo mbaya. [7] Katika barua ilyohusu mazungumzo ya baadaye Kony pia alieleza kwamba sharti angetafuuta ushauri kutoka kwa Roho Mtakatifu. Mazungumzo yalipoanza walisisitiza kwamba viongozi wa dini washirikishwe na walifungua mkutano kwa maombi yaliongozwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Dini wa LRA Bw. Jenaro Bongoni. Hatimaye katika mazungumzo ya amani ya mwaka 1994 Kony aliingia huku wanaume waliovaa majoho wakiwa mbele yake wakimyumyizia maji takatifu. [8]

Juhudi nyingi za kimataifa za kuleta amani na kukomesha utekaji nyara wa watoto na Kony na Wanamugambo wa kundi lake la Lord's Resistance Army zilifanyika kati ya 1996 na 2001. Juhudi zote zilishindwa kumaliza utekaji nyara wa watoto, ubakaji, askari-jeshi watoto mauji ya raia ikiwemo usambuliaji wa kambi za wakimbizi. Baada ya shambulizi la tarehe 11 Septemba Marekani ilitangaza rasmi wanamugambo wa Lord's Resistance Army kuwa kundi la kigaidi na Joseph Kony kuwa gaidi. [9]Josph Kony alifikiriwa kuwa mtu mwenye pepo; amesawiriwa kama ama kma Masihi au shetani. Alizuru mara kadhaa milima ya Ato nchini Uganmda. Inadaiwa kuwa angekwea hadi kileleni cha milima na kulala huko kwenye jua kali kwa siku kadhaa. Angefunikwa na kundi la kumbikumbi wekundu ambao waliing'ata ngozi yake kwa undani. Mafuta kutoka mti uitwao Yao ilipakwa mwilini mwake. Kisha aliingia kwenye pango na kushinda huko pekee kwa majuma kadhaa. Alichowaamuru watoto wafanye kilikuwa kitu cha upuzi- aliwaambia kuwa iwapo wangechora mslaba kwenye vifua vyao na mafuta wangekingwa kutoka kutoka kwa risasi. [5] Kony anasisitiza kwamba wanamugambo wa Lord's Resistance Army wanapigania Amri Kumi. "Ndiyo, tunapigania Amri Kumi," Je, ni vibbaya? siyo kukiuka haki za binadamu. Na amri haikutolewa na Joseph. Haikutolewa na LRA. la, amri hiyo ilitolewa na Mungu. " [10]

Mashtaka rasmi
Kigezo:LRA Tarehe 6 Oktoba, 2005 Mahaka ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa vibali vya kukamtwa kwa wanamugambo watano wa kundi la Lord's Resistance Amy kwa uhalifu dhidi ya haki za binadamu kufuatia kufunguliwa mashitaka. Siku iliyofuata waziri wa ulinzi wa Uganda Amama Mbabazi alidokeza kuwa Joseph Kony, naibu wake Vincent Otti na makamanda wa Raska Lukwiya, Okot Odiambo na Dominic Ongwen walikuwa miongoni mwa wale ambao vibali vyao vya kukamtwa vilitolewa. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, jeshi la Uganda lilimua Lukwiya tarehe 12 Agosti, 2006. [11]

Juma moja baadaye, tarehe 13 Oktoba, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo alitoa maelezo kuhusu mashitaka yaliyomkabili Kony. Kuna jumla ya mashtaka 33, 12 yakiwa ni uhalifu dhidi ya haki za binadamu, ambayo ni pamoja na mauaji, utumwa, utumwa wa ngono na ubakaji. Kuna mashitaka mengine 21 ya uhalifu wa kivita ambayo ni pamoja na mauaji, ukatili kwa raia, ushambulizi wa kimakusudi kwa raia, uporaji mali, ubakaji na kusajili watoto kwa nguvu katika vikosi vya waasi. Ocampo alisema kwamba "Kony aliwateka wasichana kuwatoa kama zawadi kwa makamanda wake."

Jeshi la Uganda limejaribu kumua Kony kwa shutuma za Upinzani .

Tarehe 31 Julai, 2006, Kony alikutana na viongozi kadhaa kitamaduni, kisiasa, na viongozi wa dini kutoka Kaskazini mwa Uganda mafichoni mwake katika msitu wa kondo kuzungumzia vita. Siku iliyofuata, 1 Agosti, alivuka mpaka na kuingia Sudan kuzungumza na Makamu wa Rais wa Kusini mwa Sudan Riek Machar. Baadaye Kony aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakuwa tayari kufika mbele ya mahakama ya ICC kujibu mashitaka kwa kuwa hajafanya lolote baya.

Tarehe 12 Novemba 2006 Kony alikutana na Jan Egeland, Umoja naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura. Kony aliambia shirika la habari la Reuters: "Hatuna watoto wowote. tunawapiganaji tu. [12]

Tarehe 28 Agosti mwaka 2008, wizara ya fedha ya Marekani ilimuorodhesha Kony miongoni mwa kundi la "magaidi wa kipekee duniani" kundi ambalo huwa na adhabu za kifedha na adhabu. Haijulikani iwapo Kony ana miliki au hamilki rasilimali yoyote amabyo inaathiriwa na maelezo yaliyotolewa.

Desemba 25, 2008, kwa mujibu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa, waasi wa Lord's Resistance Army (LRA) waliwaua watu 189 na kuteka nyara watoto 120 wakati wa sherehe iliyofadhiliwa na Kanisa Katoliki huko Faradje, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Desemba 2008, jeshi la Kongo, pamoja na vikosi vya jeshi la Uganda na Sudan, vilivamia waasi wa LRA wakiwa na lengo la kuwanyang'anya silaha waasi wa LRA.

No comments:

Post a Comment