KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 5, 2010

Wacharazwa Bakora Kwa Kuuza Chakula Mwezi wa Ramadhan




Wanawake wawili wa nchini Indonesia ambao walipatikana na hatia ya kuuza chakula mchana wa mwezi wa ramadhan wamecharazwa bakora mbele ya mamia ya watu.
Wanawake wawili ambao walipatikana na hatia ya kuvunja sheria za kiislamu kwa kuuza chakula wakati watu wakiwa wamefunga mwezi wa ramadhan wamecharazwa bakora mbele ya mamia ya watu waliokusanyika mbele ya msikiti.

Mamia ya watu walikusanyika mbele ya msikiti uliopo kwenye mji wa Jantho, Aceh nchini humo ili kushuhudia Murni Amris, 27 akicharazwa bakora tatu na Rukiah Abdullah, 22, akicharazwa bakora mbili.

"Hawa wanawake wawili walikamatwa wakiuza wali mchana wa mwezi wa ramadhan. Sharia za kiislamu zinapiga marufuku kuuza chakula masaa ambayo watu wanakuwa wamefunga", alisema Marzuki Abdullah mkuu wa polisi wa sharia katika jimbo la Aceh.

Bi Murni Amris alicharazwa bakora moja zaidi ya mwenzake kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mmiliki wa kibanda cha kuuza chakula wakati Bi Rukiah Abdullah alikuwa ndio mfanyakazi wake.

Walikamatwa wakiuza chakula wakati wa mwezi wa ramadhan ulioisha ambao ulianza kati ya mwezi August na septemba mwaka huu.

Gonga linki chini kwa picha zinazoonyesha wanawake hao wakicharazwa bakora.

No comments:

Post a Comment