KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 5, 2010

Jaji Rugazia auwa



JAJI Projest Rugazia, wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ameachjiwa kwa dhamana jana bada ya kushikiliwa na jeshi la polisi kutokana na kosa la kugonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo katika barabara ya Bagamoyo.
Jaji huyo alimuua Salehe Omari mkazi wa Msasani wakati jaji huyo alipokuwa akiendesha gari lake katika barabara hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, ilisema kuwa, Jaji Rugazia anatuhumiwa kusababisha kifo cha Salehe na kusababisha majeruhi watatu akatika ajali hiyo.

Kamanda Kova, alisema, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 8 usiku juzi, maeneo ya Victoria, wakati Jaji huyo alikuwa akielekea maeneo ya Kinondoni Morocco.

Alisema kuwa gari lake liliacha njia ghafla karibu na mgahawa wa Zhonghua Garden na kugonga magari yaliyokuwa yameegeshwa kando kando mwa barabara katika eneo hilo na kusababisha kifo, majeruhi na uharibifu mkubwa.

Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Issa Idd (30) mkazi wa Kinondoni, Nasibu Hassan (28), mkazi wa Kitunda na mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), aliyejulikana kwa jina moja la Rahma.

Hata hivyo Kamanda Kova alidai kuwa, Jaji huyo katika ajali hiyo alibanwa na usukani wa gari na kumsababishia maumivu sehemu za kifua, alikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuruhusiwa mara moja,kisha jeshi lake lilifika kumchukua mtuhumiwa huyo kumpelekea kituo cha polisi kwa mahojiano na baadae aliweza kuachiwa huru kwa kuwekewa dhamana

No comments:

Post a Comment