KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 11, 2010

VIDEO - Muisrael Alipowagonga na Gari Watoto Wawili wa Palestina


Ajali hii ya kutisha ilitokea baada ya kiongozi wa kikundi cha wahamiaji wa Kiisrael katika makazi ya Wapalestina mjini Jerusalem kuwagonga na gari watoto wawili wa Kipalestina baada ya watoto hao kulirushia mawe gari lake.
David Be'eri, ambaye ni mwanaharakati wa mrengo wa kulia na kiongozi wa kikundi cha wahamiaji wa Israel katika makazi ya Palestina katika kitongoji cha Silwan, mashariki mwa Jerusalem, amewagonga na gari watoto wawili wa Kipalestina ambao walikuwa wakilirushia mawe gari lake.

Katika tukio hilo lililotokea ijumaa na kunaswa LIVE na waandishi wa habari, Be'eri aliwagonga na gari watoto wawili waliosimama mbele yake. Mtoto mmoja alirushwa juu na kuangukia tumbo wakati mtoto wa pili alitupwa pembeni.

Be'eri hakusimama alikimbia toka eneo la tukio huku gari lake likiendelea kuvurumishiwa mawe na watu wengine waliokuwa eneo hilo.

Watoto hao waliwahishwa hospitali ya Moqassed Hospital mashariki mwa Jerusalem mmoja akiwa na majeraha makubwa kifuani na sehemu ya chini ya mwili wake.

Angalia VIDEO ya ajali hiyo chini.

VIDEO - Muisrael Alipowagonga na Gari Watoto Wawili wa Palestina

No comments:

Post a Comment