KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, October 12, 2010

Atinga ukweni kulalamikia kipigo kutoka kwa mkewe
MWANAUME mmoja[35] mkazi wa Mwananyamala Kisiwani [jina linahifadhiwa] ameamua kwenda ukweni kumshitaki mke wake kutokana na kipigo anachokipata kutoka kwake.
Ilidaiwa na mmoja wa ndugu wa karibu na mwanaume huyu kuwa, mke wake aliyetambulika kwa jina moja Grace [27] alikuwa akimpa kipigo pindi anapomkera na yeye kudaiwa alikuwa akihofia kumpiga kwa kuhofia kumjeruhi.

Ilidaiwa kuwa alishawahi kupata kipigo kwa takribani mara mbili na kipigo cha mwishoni mwa wiki iliyopita ilidaiwa kuwa uvumilivu ulimshinda na kwenda kuripoti matukio hayo ukweni ili mke wake huyo aweze kurekebishwa.

Hata hivyo chanzo cha habari hii kilidai kuwa, ndugu wakaribu walipomuuliza alikuwa anapigwa kwa kuzidiwa nguvu na mke wake huyo au ni kwa vipi? Mwanaume huyo aliwajibu kuwa hazidiwi nguvu ila kwa kuwa anampenda sana mke wake alikuwa anahofia kumpiga kwa kuwa angeweza kumjeruhi hivyo anaamua amuache tu.

Hivyo taarifa hiyo imeshafika ukweni na wazee wa familia wanapanga siku ya kukutana kumkanya binti yao huyo na kitakachojiri kitawajia zaidi

No comments:

Post a Comment