KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 11, 2010

SAHRINGON yataka adhabu ya kifo ifutwe



Mtandao wa Mashirika ya Haki za Binadamu, Kusini mwa AfriKa, Tawi la Tanzania (SAHRINGON) umeitaka serikali kukubaliana na mkataba wa nyongeza wa haki za kiraia unaoziagiza nchi kufuta adhabu ya kifo.
MTandao huo unapinga vikali adhabu ya kifo na kuitaka Tanzania kuiunga mkono mkataba huo ili adhabu hiyo isitaumike.
Ulisema kuwa adhabu hiyo inalenga ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu hivyo ipingwe vikali kwani hata sheria za haki ya mwanadamu inapinga adhabu hiyo.

Katika Takwimu zilizotolewa zilisema zaidi ya nchi 137 ya nchi zote duniani tayari zimeshafuta kabisa adhabu hiyo ya kifo ispokuwa nchi zipatazo 63 ikiwemo na Tanzania bado haijafuta adhabu hiyo.

Hivyo mtandao huo uliitaka Tanzania nayo iungane na nchdi zingene zilizofuta adhabu hiyo kwani adhabu hiyo ni ya kikatili na uwepo wake haipunguzi makosa ya jinai

No comments:

Post a Comment