KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, October 13, 2010

Ujumbe wasababisha talakaMWANAMKE mmoja [jina kapuni]mkazi wa Mtoni, juzi amejikuta akiandikiwa talaka ya ghafla baada ya kudaiwa kumkera mamda yake mkwe kwa kumuandikia ujumbe wa simu uliuofanya apewe talaka hiyo na mume wake.


Ujumbe huo ulisema kuwa “ mama naomba usituingilie mambo yetu ya ndani mimi na mume wangu, angalia maisha yako nasi tuachie wenyewe” haihusu kutufatilia” ulimaliza ujumbe huo

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alimtumia ujumbe mama yake mkwe baada ya kuona mama huyo yuko kwenye maamuzi ya juu kuhusiana na maisha yao ya ndoa jambo ambalo yeye haliafiki.

Hata hivyo imedaiwa kuwa jambo lolote linalohusiana na ndoa yao mume wake huwa analifikisha kwanza kwa mama yake huyo ndipo atolee maamuzi.

Baada ya ujumbe huo kumfikia mama huyo alighadhibika na kumuonyesha ujumbe huo mwanae kipenzi na mwanae kuchukua uamuzi wa kumpa talaka kwa madai alimdharau mama yake

No comments:

Post a Comment