KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, October 13, 2010

Ataka kujiua kwa kukerwa na mchumbaMSICHANA mmoja mkazi wa Kibaha, Pwani, jana alinusurika kifo baada ya kukutwa akiwa katika hatua za mwisho za kunywa vidonge aina ya mseto kwa madai alitaka kujimaliza kutokana kuudhiwa na mume wake mtarajiwa.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 24,mwenye taaluma ya ualimu alikuwa amedhamiria kuzidisha kunywa vidonge vya kutibu malaria aina ya mseto pakti mbili na kuwahiwa na ndugu walioingia chumbani humo.

Ilidaiwa na ndugu wa karibu wa msichana huyo kuwa, msichana huyo alikerwa na tabia ya mchumba wake ambaye aliwadokezea kuwa mchumba wake alikuwa na tabia ya kumuomba amuingilie kinyume na maumbile na yeye hakuafiki tabia na kudai kuwa labda alikuwa akimtania.

Ilidaiwa kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita msichana huyo alitaka kuthibitisha kama ni kweli alidhamiria ama alikuwa anamtania, na aliamua kumtania na alipothibitisha kuwa alikuwa hamtanii alisitisha na kumuamuru aende akachukue mahari yake aliyoitoa nyumbani kwao.

Hivyo kwa kuwa mchumba huyo alishatambulishwa nyumbani na kutoa nusu ya mahari, aliamua awaambie baadhi ya dada zake na kuwambia hakuwa tayari kuolewa tena na mchumba huyo na kuwaelea bayana aliyokuwa akiyahitaji mchumba wake.

Kutokana na kusitisha uchumba huo ambayo wachumba hao walikuwa wanatarajia kufunga ndoa Desemba mwaka huu, aliona kwa kutiwa aibu na mchumba huyo na alichukua uamuzi huo wa kujiondoa maisha kutokana na aibu hiyo.

Hata hivvyo mchumba huyo hakuwa tayari kumuacha msichana huyo na kumwambia ni lazima amuoe na tabia hiyo asingeiendeleza kwani alikuwa akimpima kama alikuwa anashiriki vitendo hivyo.

Hata hivyo msichana huyo alishikwa na uogaa na kumwambia hayuko tayari kuolea naye tena kwa hofu.

Ilidaiwa kuwa mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina moja Eddo nae hakutaka kupata aibu kwa upande wake anaendelea kumbembeleza mchumba wake huyo ili waweze kufunga ndoa.


Msichana huyo aliwahishwa kwenye zahanati ya karibu na hali yake inaendelea vizuri
muendelezo wa habari utaendelea

No comments:

Post a Comment