KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 9, 2010

Udhalilishaji wa wanafunzi Kenya waanikwa




Wanafunzi wa kike Kenya

Zaidi ya walimu 1,000 wamefukuzwa kazi nchini Kenya kwa kuwadhalilisha mabinti katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Afisa mwandamizi wa serikali Ahmed Hussein aliiambia BBC kuwa wengi walioathirika ni wa kati ya umri wa miaka 12 hadi 15.

Alisema kupitia simu iliyowekwa mahsusi ambapo watu hupiga kutaka ushauri kwa siri kusaidia waathirika imeonyesha tatizo hilo ni kubwa zaidi kuliko ilivyodhaniwa hapo awali.

Matukio hayo yametokea zaidi katika shule za msingi maeneo ya vijijini.

Mahakama imemtia hatiani?
Bw Hussein, kutoka wizara ya Jinsia, Watoto na Maendeleo ya Kijamii aliiambia BBC, " Awali hatukuweza kujua kinachotokea nchini kutokana na mawasiliano mabaya, lakini kwa sasa mawasiliano yako kote- kuna simu za mkononi nchini kote."

Mwaka jana, walimu wa kiume 600 walifukuzwa na mpaka sasa kwa mwaka huu pekee walimu 550 wamepoteza kazi zao kwa kosa la kubusu, kugusa, au kuwatia mimba watoto wa kike kutoka kwa walimu 240,000 nchi nzima.

Bw Hussein alisema, " Idadi kubwa ya walimu hao wamefikishwa mahakamani, na kuhukumiwa kulingana na sheria."

Brian Weke, mkurugenzi wa mpango wa Cradle, wakfu wa haki za watoto Kenya, alikubali kuwa tatizo limeenea.

Alitoa mfano wa tukio moja lililotokea katika jimbo la Nyanza mwaka jana: " Niligundua katika shule moja ya msingi tulikuta zaidi ya watoto 20 walikuwa wajawazito na takriban nusu ya idadi hiyo walitiwa mimba na walimu wenyewe."

Hata hivyo, alisema maafisa wanaofanya uchunguzi wa udhalilishaji huo hawakuwa wakitoa taarifa za msingi za kuweza kuwatia hatiani.

Bw Weke aliiambia BBC, " Tatizo letu kubwa ni kwamba maafisa wa elimu wa wilaya- hawafikshi taarifa hizi kwa polisi."

Mwandishi wa BBC Will Ross aliyopo Nairobi, alisema walimu aghalabu wanaokutwa kuwanajisi wanafunzi wao huishia kuwalipa wazazi ili kuzuia kesi hizo kufikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment