KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, October 9, 2010
Idadi ya wahamiaji yapungua katika nchi tajiri
Kwa takriban miongo mitatu kuhama kutoka nchi maskini kwenda nchi tajiri kulikuwa kumekithiri,lakini sasa hali ni tofauti kwa kuwa uhamiaji huu umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na mdororo wa uchumi duniani.
Kutokana na utafiti uliofanywa na BBC unaonyesha wahamiaji ndiyo wanaokumbwa na tatizo hili zaidi,lakini ukaongeza kuwa mabilioni ya pesa wanayotuma nyumbani kwa jamii zao kila mwaka bado yanaendelea vile vile.
Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa idadi ya wahamiaji katika nchi tajiri iliongezeka kutoka asilimia tano hadi kumi kati ya mwaka 1980 na 2010.Lakini utafiti huu mpya uliofanywa na BBC kupitia taasisi ya sera za uhamiaji ilio na makao yake Washington,Marekani unasema msukosuko wa uchumi duniani umewaathiri wahamiaji zaidi.
Hii ni kutokana kuwa wahamiaji wengi hawana utaalamu katika sekta za uchumi kama vile ile ya ujenzi ambayo haifanyi vizuri wakati uchumi unapokuwa na msukosuko.
Katika nchi zengine idadi ya wahamiaji imepungua sana-idadi ya wahamiaji wanaoingia Uhispania ilipungua kwa thuluthi mbili mwaka 2009, na Ireland na Ugiriki ambazo zinafahamika kwa kupokea wahamiaji kwa ajili ya kufanya kazi kwao,zinaweza kuwa nchi ambazo watu wanaondoka kwenda kutafuta ajira nje.
Lakini kama mdororo wa uchumi,na sheria kali za uhamiaji,zimepunguza wahamiaji kutoka nchi zinazoendelea hadi nchi tajiri,pesa ambazo wahamiaji wanatuma kwao bado hazijapungua.Inaonekana kuwepo au kusiwepo na mdororo wa uchumi,wakati unapotaka kutuma pesa kwa watoto wako au mama yako,utafanikiwa tu kupata njia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment