KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 9, 2010

Sokwe mvuta sigara afa Afrika Kusini





Sokwe aliyepata umaarufu mkubwa kwa uraibu wake wa kuvuta sigara amefariki dunia huko Afrika Kusini akiwa na miaka 52.

Sokwe huyo aliyepewa jina Charlie alianza kuvuta sigara baada ya watalii waliotembelea hifadhi ya wanyama ya Mangaung huko Bloemfontein kumtupia sigara iliyokuwa imewashwa.

Msemaji wa hifadhi hiyo Qondile Khedama alisema sokwe huyo alipata umaarufu mkubwa akiwatumbuiza maelfu ya watalii kila mwaka.


Sokwe huyo anafanyiwa upasuaji ili kubaini kilichomwuua.

Kwa miaka mingi wafanyakazi kwenye hifadhi ya Mangaung wamekuwa wakijaribu kumsaidia sokwe huyo kufutilia mbali uraibu huo na hata kuwaonya watu wasimpe sigara.

Qondile Khedama amesema itakuwa vigumu sana kumpata sokwe mwingine mwenye sifa kama za Charlie.





Hata hivyo msemaji huyo wa hifadhi ya Mangaung amenukuliwa akisema hadhani uvutaji wa sigara ulikatisha maisha ya Charlie akiongezea kusema kuwa aliishi miaka kumi zaidi ya maisha ya kawaida ya sokwe.

Sokwe huyo alikuwa anapokea matibabu ya hali ya juu pamoja na chakula maalum kulingana na Khedama.

Mwezi Februari iliripotiwa kuwa sokwe mwingine nchini Urusi alipelekwa kwenye hifadhi ya kurekebisha tabia baada ya kuwasumbua wageni akitaka kupewa pombe na sigara.

No comments:

Post a Comment