KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, October 14, 2010

Tufate mazuri ya mwalimu, tusiipeleke nchi pabaya



RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, ametoa angalizo kwa Watanzania kwa kuwataka wafuate wosia wa alioacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili wasiipeleke nchi mahali pabaya.
Rai hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho ya kuadhimisha miaka 11 toka kutokea kifo cha cha muasisi huyo.

Alisema watanzania wanatakiwa wawe makini ili kuendeleza amani iliyopo nchini kw a kufuata wosia aliotuachia la sivyo nchi inaaenda pabaya.

Mwinyi aliwakumbusha watanzania kuwa wakati wa uhai wa baba wa taifa, mwalimu alikemea kabisa ukabila na kupiga vita udini hakuruhusu viwepo nchini kwa kuwa alikuwa andaona athari za ubaguzi huo.

Pia mwalimu aliwataka watanzania wawe wamoja wasibaguane ikiwemo na nkujeng a umoja wa kimataifa, kutoruhusu matumizi mabaya ya fedha za serikali, rushwa ambako hivi sasa vinaonekana kuwepo kwa asilimia kadhaa kwaw watanzania.

Mwinyi aliwakumbusha watanzania kuwa katika mabaya hayo mwalimu Nyerere aliviogopa kama ukoma kwa kuwa vingeweza kuangamiza nchi.

Aliwakumbusha “watanzania tuendeleza wosia wake na nchi itabaki kwa amani, pia tuchague viongozi bora kufuata sera na kuachana na kumchagua mtu kufuata dini ya mgombea hii inaweza ikalipeleka taifa pabaya” alimalizia Mwinyi

No comments:

Post a Comment