KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, October 14, 2010
Polisi yaendelea na uchunguzi tuhuma juu ya Mengi
KUFUATIA na malalamiko yaliyotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Bw. Reginald Mengi kutuhumu baadhi ya askari, jeshi hilo limeunda tume maalum kuchunguza malalamiko hayo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mengi kutamka hadharani kuwa kuna maofisa wa polisi walitaka kumbambikizia dawa za kulevyaa mwanae, Abdiel Mengi alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa MWalimu Nyerere.
Mengi alitoa na kufichua njama dhidi ya maofisa hao juzi alipowasilisha habari hiyo kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Mengi aliwataja maofisa watatu waliotaka kumbambikizia dawa hizo kuwa ni, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya pia ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, Bw. Godfrey Nzowa, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Charles Mkumbo na askari mwingine mmoja wa aliyemtaja kwa jina la Hendry.
Mengi alibainisha kuwa maafisa hao aliunda njama kumchafua mwanae kwa kuahidiwa kupewa shilingi milioni 15.
Hivyo kufuatia tuhuma hizo IGP Saidi Mwema alisema jana kuwa, wameunda timu maalumu itakayoongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Jinai, (DCI), Robert Manumba..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment