KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, October 14, 2010

Kama Una Moyo Mwepesi ..?Kama kuna watu ambao hawahisi maumivu miili yao inapotobolewa na visu, bisibisi, majembe na vitu vingine vyenye ncha kali basi watu hao si wengine bali wafuasi wa dini ya watu wasiokula nyama ya nchini Thailand. Kama una moyo mwepesi usiangalie picha zifuatazo.
Tamasha la dini ya watu wasiokula nyama (vegetarian) limeanza nchini Thailand ambapo wafuasi wa dini hiyo wamekuwa wakijichoma kwa vitu mbalimbali vyenye ncha kali wakiamini wanaitoa mikosi toka kwenye miili yao na kuieletea bahati njema jamii yao.

Tamasha hilo la siku tisa lina historia ndefu ambapo kwa mara ya kwanza lilifanyika kwenye miaka ya 1800.

Wafuasi wa dini hiyo wamekuwa wakikusanyika kwenye mji wa Phuket nchini Thailand na wamekuwa wakiitoboa miili yao na kujichomeka vitu mbali mbali kuanzia majembe, mapanga na vinginevyo.

Kama una moyo mwepesi usiclick linki chini kuangalia picha za tamasha hilo mwaka huu.

No comments:

Post a Comment