KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 5, 2010

Tendwa atoa onyo kwa Shekhe Yahaya, Kakobe


MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, ametoa onyo kwa viongozi wa dini wanajimu wanaojihusisha na kutabiri mambo yanayohusiana na uchaguzi mkuu kitendo ambacho amesema kinahatarisha na kuvuruga amani.
Msajili huyo amesema kuwa viongozi hao wamekuwa wakijihusishwa na shughuli za utabiri wa hapa na pale na kusema vitendo hivyo vinaweza vikahatarisha amani ya nchi kutokana na utabiri huo.

Tendwa aliwataja viongozi hao hadharani mbele ya waandishi wa habari na kusema viongozi hao ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship , Zacharia Kakobe na Mtabiri na mnadhimu wa nyota maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein.

Tendwa amesema, kuwa watu hao ni hatari na wanaweza kuvuruga amani ya nchi kwa utabiri wao ambao hauna misingi na mafundisho yoyote wanaoutoa kila kukicha kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao tarajio na taarifa hizo kusikika na wapiga kura hali ambayo inaweza kuleta fujo.

Hivyo aliwataka viongozi hao kuendelea na shughuli zao za elimu ya kiroho na kuachana na kuepukana na siasa kwani wanaweza kuhatarisha amani ya nchi na kukemea vitendo vya kakobe kutoa elimu ya uraia kanisani kwake.

Pia alimuonya Sheikh Yahya kurusha vipindi vyake vya utabiri katika kituo cha television kuhusiana na uchaguzi na kuonekana kukipigia debe chama kimoja kinachoshiriki katika uchaguzi huo.

Hivyo Tendwa ameonekana kukemea vikali vitendo hivo na kuahidi kutunga sheria kali kuhusiana na vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment