KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, October 5, 2010

Mtoto afa baada ya kuwasha kibiriti chumbaniMTOTO Warda Mohamed [3] amefariki dunia kwa ajali ya moto baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuungua na moto huko Tabata Bonde la Msimbazi.
Kamanda wa Polisi Ilala, Faustine Shilogile alisema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi wakati mtoto huyo akiwa chumbani alipochezea kiberiti.

Kitendo hicho kilisababisha moto mkubwa uliopelekea nyumba nzima kuteketea huku mtoto huyo akiwa ndani.

Kamanda Shilogile alisema kuwa mtoto huyo alipoteza maisha katika eneo la tukio.

Katika tukio jingine lililotokea jijini Dar es Salaam, Wilson Danford [27] mkazi wa Mabibo Ushere amekutwa akiwa amekufa chumbani kwake.

Chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika uchunguzi unaendelea

No comments:

Post a Comment