KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 9, 2010

Askofu Desmond Tutu astaafu shughuli za umma



Mmoja wa mashujaa wa harakati kupinga ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, Askofu Desmond Tutu anasherekea miaka 79 ya kuzaliwa kwake hii leo na siku hii pia itakuwa yake ya kustaafu kutoka shughuli za umma.

Mzee Tutu anasema anatoa nafasi kwa vizazi vipya kuongoza. Katika harakati zake kupinga ubaguzi wa Rangi Tutu alihudumu pia kama askofu mkuu wa jimbo la Cape Town na baada ya uhuru wa Afrika Kusini akateuliwa kuongoza tume ya haki na maridhiano.

Tume hii ilichunguza uhalifu uliotikelezwa katika enzi ya ubaguzi wa rangi. Mwaka 1984 mtetezi huyo wa haki za kibinadamu akashinda tuzo ya amani ya Nobel.


Askofu Desmond Tutu kwa wengi ni msingi wa maadili katika jamii. Katika huduma yake akiwa kasisi wa kiangilikana miaka ya 70 Mzee Tutu alikua sauti iliyopinga ubaguzi wa rangi.

Kampeini zake dhidi ya utawala wa makaburu aliiplekeka katika makaazi ya waafrika weusi miaka ya 80. Kwa wakati mmoja aliwatuliza raia waliokuwa wakitaka kumteketeza polisi mzungu.

Katika miaka ya Karibuni amehusika pia katika kutatua mizozo. Aidha pia alijipata katika masuala yaliyozua utata hususan alipomkosoa hadharani rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na Aliyekuwa Waziri Mkuu Uingreza Tony Blair.

Katika buriani yake, Askofu Tutu alisema," Tarehe saba mwezi Okotoba natimiza miaka 79, siku hii pia nastaafu kutoka kwa umma. Sitafanya tena vikao na wanahabari. Maisha yangu sasa ni kupumzika na mke wangu tukitizama mechi za soka, Kriketi na raga. Kisha nitakuwa nikiwatembelea wangangu na wajukuu wangu, badala ya kufanya mijadala au kutoa hotuba katika vyuo vikuu".

Japo anastaafu, Desmond Tutu atasalia mfano wa kujivunia nchini Afrika Kusini

No comments:

Post a Comment