KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 11, 2010

TCRA hatuhusiki, wawarushia mpira kampuni za simu




MAMLAKA ya Mawasiliano nchini [TCRA] imesema hawahusiki moja kwa moja na sakata la urushaji ujumbe mfupi katika simu za viganjani za kumchafua Dk.Slaa na kuambia chama hicho kuwa hilo ni suala linalohu mitandao ya simu.


Hayo yamekuja ni baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] kupanga kuwasilisha malalamiko kwenye vyombo vya dola kuhusiana na usambazaji wa ujumbe huo katika simu za viganjani.

Hivyo chamda hicho wamekiita kitendo hicho ni uchochezi na utaleta umwagaji wa damu nchini hivy0 taarifa hiyo imeshawasilishwa polisi kwenye vyombo vya usalama.

Akizungumzia suala hilo, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, amesema, maneno ya ujumbe huo yanashabihiana na uyale aliyoyasema Mwenyekiti wa Kampeni wa CCM, Bw. Abdulrahman Kinana.

UJumbe unaosambazwa hivi sasa katika simu za mkononi kwa watu tofautitofauti unaotoka kwenye namba +3588976578 Ujumbe huo “Slaa ni mropokaji na mgomvi anayelumbana na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi, anataka damu imwagike ili mradi apate ushindi. Hana uwezo wala sifa ya kuwa Rais. Tumwepuke Slaa kama ukoma. Tusidanganyike.” Unasema ujumbe huo

No comments:

Post a Comment