KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, October 14, 2010

Juhudi za kuachiliwa kwa mateka Muingereza zaendelea SomaliaWapiganaji Wakisomali

Wazee wa jadi nchini Somalia wamesema wanajadiliana na watekaji nyara wa raia wa Uingereza aliyetekwa karibu na mpaka wa Ethiopia wiki hii.

Wazee hao walimwambia mwandishi wa BBC kuwa waliwazuiwa watekaji nyara kumkabidhi mateka huyo kwa wanamgambo wa Kiislam.

Kwa wakati huu wazee hao wanawashinikiza watekaji nyara kumwachilia huru mateka huyo.

Mateka huyo, ambaye pia ana uraia wa Zimbabwe, alikuwa mfanyakazi wa shirika la misaada la Save the Children.

Mfanyakazi mwingine raia Wakisomali ambaye naye alitekwa nyara pamoja na Muingereza huyo aliachiliwa huru bila madhara yoyote.

No comments:

Post a Comment