KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 9, 2010

Mlinda amani wa Darfur atekwa nyara



Mwanajeshi wa kulinda amani katika jimbo la Darfur, Sudan ametekwa nyara. Hii ni kwa mujibu wa kikosi cha kimataifa kinacholinda amani eneo hilo.

Tukio hilo limetokea mjini El Fasher ambapo ujumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unazuru kutathmini shughuli za amani ya Darfur.

Kwa mujibu wa wanajeshi wa kulinda amani, watu kadhaa waliojihami walivamia nyumba ya wajumbe wa UNAMID.Wanaume wawili walifungwa kwa kamba na wenzao wawili wakatekwa.Mmoja wa waliotekwa aliweza kutoroka baadaye lakini mwenzake mmoja hakufanikiwa.

Kumekuwa na matukio kadhaa ya raia wa kigeni kutekwa nyara tangu mahakama ya uhalifu ya kivita ya The Hague ilipotangaza kuwa Rais Omar Al Bashir anatakiwa kujibu mashtaka kadhaa ikiwa ni pamoja na mauaji ya kimbari huko Darfur na ukiukwaji wa haki za kibinadamu,wengi ya wateka nyara wakiwa na nia ya kupata pesa.

Lakini utekwaji huu ambao umetokea katika mji ule ule wanaokaa wajumbe wa baraza la usalama,litatia wasiwasi mkubwa vikosi vya kulinda amani vya UNAMID.

Tayari wajumbe hao wa baraza la usalama hawajapata makaribisho ya kuridhisha kutoka kwa wale wanaomuunga mkono rais Bashir,kufwatia baadhi ya wajumbe hao kukataa kukutana naye.

Pia kumetokea mapigano mengine huko Darfur hapo jana. Majeshi ya Sudan yamesema kwamba yameweza kuchukua udhibiti wa eneo moja linalojulikana kama Suni, na kufanikiwa kuwafukuza waasi.Waasi hao kundi la Abdel Wahid wanasema walishambuliwa kwa ndege na raia wengi waliuawa.Jeshi la Sudan limekanusha hilo.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaendelea huko Darfur , magharibi mwa Sudan lakini kwa sasa macho yote yako kwenye kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika januari mwaka ujao

No comments:

Post a Comment