KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 9, 2010

Kesi ya Lubanga itaanza upya ICC



Chombo kinachoshughulikia rufaa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kimeamua kuwa kesi ya mbabe wa kivita ianze upya baada ya kusimamishwa kwa miezi mitatu.

Mwezi Julai, majaji waliisimamisha kesi ya Thomas Lubanga kuhusu makosa ya uhalifu wa kivita na kuamuru aachiliwe huru baada ya waendesha mashtaka kukataa kuwasilisha taarifa kwa upande wa utetezi.


Thomas Lubanga


Hukumu ya Ijumaa ilibadili uamuzi, lakini pia kumshutumu mwendesha mashtaka Luis Moreno Ocampo kwa kudharau amri za mahakama.

Bw Lubanga amekana kutumia watoto kama wanajeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia mwaka 2002 hadi 2003.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 49 aliongoza Union of Congolese Patriots, UPC, wapiganaji wa kabila la Hema, moja ya makundi sita yaliyopigana ili kudhibiti mkoa wa Ituri.

Ghasia za kugombea ardhi ziligeuka na kuwa vita vya kikabila ambapo takriban watu 50,000 waliuawa na maelfu walibaki bila makazi

No comments:

Post a Comment