KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, October 9, 2010

Mama Anawezaje Kumfanyia Hivi Mwanae kweli?


.
Mama mmoja wa nchini Marekani na mpenzi wake wametupwa jela baada ya kuwaonyesha watu picha wakiwa wamembandika ukutani kwa kutumia gundi ya plastiki mtoto wao.
Jayla Hamm, 18, na mpenzi wake Corde Honea, 19, walimbandika ukutani kwa kutumia gundi ya plastiki mtoto mwenye umri miezi 22 huku wakimpiga picha na kumcheka jinsi alivyokuwa akihangaika.

Walimpiga picha pia wakiwa wameking'iniza juu kwenye ukuta kikombe chake cha kinyaji alichokuwa akikipenda sana huku mtoto huyo akihangaika kukifikia bila mafanikio.

Picha nyingine ilimuonyesha mama huyo na mpenzi wake wakicheka huku mikono ya mtoto huyo ikiwa imefungwa kwa gundi ya plastiki.

Polisi wa Lincoln, Nebraska, ambao walishtushwa sana na tukio hilo walisema kuwa Jayla na mpenzi wake walikuwa wamelewa sana baada ya kurudi toka kumbi za starehe, walimtumia mtoto huyo kama njia yao ya kujiburudisha.

Jayla amehukumiwa kwenda jela siku 10 kwa uzembe wa kumtelekeza mtoto wake wakati Corde Honea alihukumiwa kwenda jela kati ya miaka mitatu na mitano kwa kumtesa mtoto huyo.

Jayla amenyang'anywa mtoto wake ambaye sasa atalelewa na serikali.

No comments:

Post a Comment