KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 9, 2010

Kweli Hasira Hasara

Wahenga hawakukosea kamwe waliposema hasira hasara, picha hii inamuonyesha mlemavu wa miguu wa nchini Korea anayeendesha baiskeli ya umeme ya walemavu akipoteza maisha yake kutokana na hasira zake baada ya mlango wa lifti kujifunga kabla hajaufikia.
Mwanaume wa nchini Korea Kusini aliyejulikana kwa jina la Mr Lee mwenye umri wa miaka 40 ameiaga dunia baada ya kushindwa kuzidhibiti hasira zake.

Mr Lee ambaye ni mlemavu wa miguu anayetumia baiskeli ya umeme, alishikwa na hasira baada ya mlango wa lifti katika shopping mall katika mji wa Daejon kujifunga kabla hajaufikia.

Hasira za Mr Lee zilimtuma atumie baiskeli yake kuugonga mlango wa lifti.

Aliugonga mara ya kwanza hakuna kilichotokea, alirudi nyuma na kuugonga tena na kusababisha mlango wa lifti uanze kubomoka, aliporudi nyuma na kuugonga kwa mara ya tatu mlango huo ulibomoka kwa chini na kupelekea Mr Lee atumbikie ndani na kuporomoka chini mita 6 na kupelekea kifo chake.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa Mr Lee alikasirika kwanini mwanamke aliyekuwa ndani ya lifti hakuizuia lifti kujifunga milango yake

No comments:

Post a Comment