KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 13, 2010

Maandalizi yakamilika karatasi za kura zaingia nchini



TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema zaidi ya nusu ya karatasi za kupigia kura zimeshawasili nchini kutoka nchini Uingereza zilipokuwa zinachapishwa.


Mkurugenzi wa tume hiyo, Bw. Rajabu Kiravu alitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam.

Kiravu alisema, maandalizi yote yameshakamilika na linasubiriwa zoezi la upigaji kura lifike na tayari karatasi hizo zimeshawasili nchini kutoka kampuni ya zabuni ya Kalamazoo Secure Solutions ya Uingereza zilipokuwa zikichapwa.

Hata hivyo alisema kwa mwaka huu, mfumo wa karatasi hizo umebadilika na kuacha muundo ule wa zamani.

Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktob 31 nchini kote ambako watanzania watachagua viongozi wa kuwaongoza kwa miaka mitano ijayo ka kuridhihwa na sera zao ambako agombea bado wanaendelea kujinadi majimboni katika kuelekea kuomba ridhaa ya wananchi.

Tayari tumeshasikia wagombea wa urais wakitoa ahadi zao huku kila mmoja akiahidi ahadi zake, tumeshasiki Mgombea urais [CCM] Jakaya Kikwete akiahidi vyuo vikuu, mgombea urais [CUF] Ibrahim Lipumba kuahidi elimu bure na wa Chadema, Wilbrork Slaa kuahidi vilevile akipata ridhaa elimu itakuwa bure na hadi nyingi.

Uchaguzi wa mwaka huu umeingia na hofu kwa watanzania, kuonekana kuwa kuna dalili za udini ndani yake huku viongozi wa dini wakiwaasa watanzania kumchagua mgombea kufuata sera zake na kuacha udini ili kuendeleza amani iliyopo

No comments:

Post a Comment