KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 9, 2010

Mkuu wa benki atupwa jela Nigeria




Sarafu ya Nigeria - Naira


Mkuu wa zamani wa benki nchini Nigeria amehukumiwa kwenda jela kwa miezi sita kwa makosa ya udanganyifu na pia kutakiwa kurejesha zaidi ya dola bilioni 1.2 taslimu na amana.





Cecilia Ibru, ambaye alikuwa mkurugenzi mkuuwa benki ya Oceanic, alikiri makosa matatu kati ya 25 ya udanganyifu na utawala mbovu.

Bi. Ibru ni mmoja kati ya wakuu kadhaa wanaoshikiliwa kuhusiana na hatua ya karibu kuporomoka kwa beki tisa mwaka 2009.

Mwandishi wa BBC mjini Abuja, Caroline Duffield amesema hukumu hiyo imetikisa sekta ya kifedha nchini Nigeria.

Hukumu ya Bi. Ibru imefuatia makubaliano ya kisheria, amesema Jaji Dan Abutu akiiambia mahakama mjini Lagos siku ya Ijumaa.

Hukumu zake tatu ni za miezi sita kila moja, lakini zitaenda sambamba. Hii inamaanisha atakaa gerezani kwa miezi sita tu, anasema mwandishi wa BBC.

"Hii ni ishara kuwa tunapiga hatua katika vita dhidi ya ufisadi nchini," amesema Farida Waziri, ambaye ni mkuu wa shirika la kupambana na ufisadi nchini Nigeria, katika taarifa aliyotoa.

Serikali ilimuondoa Bi. Ibru pamoja na wakurugenzi wengine kutoka katika taasisi kadhaa za kifedha mwaka 2009.

Benki kuu ililazimika kuingilia kati na kuzikomboa benki tisa ambazo zilikuwa almanusura ziporomoke kutokana na utoaji mikopo hovyo na udanganyifu.

Bi. Ibru anatoka katika tabaka la watu wenye uwezo mkubwa kifedha, ambao humiliki biashara kubwa nchini humo. Mwandishi wa BBC anasema alikuwa maarufu katika kutokana na uvaaji wake wa vito na pia kupenda kutumia ndege binafsi.

Mpaka kukamatwa kwake, Bi Ibru alionekana kama mtu asiyeweza kuguswa na mkono wa sheria, ameeleza mwandishi wetu.

Hata hivyo, wakosoaji wanasema kesi chache sana ndio zinasikilizwa

No comments:

Post a Comment