KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 6, 2010

Kesi ya Chenge yaanza kwa utetezi



MSHITAKIWA katika kesi ya kuua na kuendesha gari kizembe inayomkabili mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi Magharibi [CCM], Andrew Chenge, jana alikana shtaka la kuendesha gari bila kuwa na bima
Jana kesi hiyo ilianza kusikilizwa mahakamani na mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na kujitetea mbele ya mahakama kuwa ajali hiyo ilisababishwa na dereva wa bajaji kutokana na kuhama upande wake.

Utetezi huo ulianza jana mbele ya hakimu Kwey Rusema wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ya jijini Dar esSalaam.

Alijitetea kuwa, alijaribu kumkwepa dereva huyo kwa kwenda upande wa kulia, lakini alishindwa kwa sababu kulikuwa na gari nyingine ilikuwa inakuja na kuwa angetoka zaidi angesababisha ajali nyingine zaidi.

Pia alikana kuwa ushahidi ulipotolewa na shahidi wa pili waliodai kuwa waligongana uso kwa uso na bajaji si kweli na kudai alitoa ushahidi huo kwa kuwa alikuwa na bifu nae.

Chenge alikana mahakamani hapo gari lake kutokuwa na bima na kueleza kuwa kitu hicho hakiwezekani kwa kuwa mke wake anafanya kazi katika ofisi inayoshughulika na ukataji wa leseni na mke wake huwa anamkumbusha mara kwa mara.

Awali Chenge alipandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya kuendesha gari kwa uzembe na pia kuendesha gari hilo bila bima na kusababisha vifo vya watu wawili.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 20, mwaka huu

No comments:

Post a Comment