KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 6, 2010

Kuelekea uchaguzi mkuu mashehe wanena



JANA Jopo la mashehe wa dini ya Kiislamu,walikutana kujadili na kuwaasa watanzania kuchagua viongozi wenye sifa bora na si kwa kuangalia udini.
Mufti Issa Shaaban bin Simba aliongoza mjadala huo na kuwaonya watanzania kutengeneza Tanzania iliyo bora na si kuangalia itikadi za kidini.

Hayo yamekuja baada ya baadhi ya viongozi wa kidini nchini kuwausia waumini wao kuchagua viongozi wa dini zao na hali hiyo inaweza kuigawa nchi kwa matabaka ya kidini.





"Watanzania tunaomba mpige kura mwaka huu kuchagua viongozi kwa misingi ya sera na si dini zao" walisisitiza.

Simba alisema wameamua kuitisha kikao hicho kwa kuwa kuna vuguvugu ya kushawishi wapiga kura kwa misingi ya kidini

Jopo hilo liliwataka wananchi kwa ujumla wakatae kupotoshwa na viongozi wa dini na wachague kiongozi kulingana na sera zake na utendaji wake atakapochaguliwa

No comments:

Post a Comment