KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, October 14, 2010

Ajitokeza Uchi Mbele ya Obama, Ashinda Dola Milioni 1Juan James Rodriguez alipotiwa mbaroni na polisi baada ya kujitokeza mbele ya rais Obama akiwa uchi wa mnyamaMwanaume ambaye alijitokeza mbele ya rais wa Marekani, Barack Obama akiwa uchi wa mnyama huku akiwa na maandishi ya kutangaza tovuti ya bilionea Alki David, amejishindia zawadi ya dola milioni 1 toka kwa bilionea huyo.
Juan James Rodriguez, 24, alitiwa mbaroni na polisi baada ya kujitokeza mbele ya rais wa Marekani, Barack Obama akiwa uchi wa mnyama huku akiwa na maandishi makubwa kifuani na tumboni ya kutangaza tovuti ya bilionea Alki David.

Rais Obama alikuwa Philadelphia akikipigia kampeni chama chake wakati Juan alipojitokeza mbele yake ghafla akiwa uchi wa mnyama.

Bilionea Alki, Mgiriki aliyezaliwa Lagos, Nigeria alitangaza zawadi ya dola milioni moja kwa mtu yoyote atakayejitokeza uchi wa mnyama mbele ya rais Obama huku akiwa na maandishi ya kutangaza tovuti ya bilionea huyo inayoitwa “BATTLECAM”.

Akiongea na waandishi wa habari, bilionea huyo alisema kuwa atatimiza ahadi yake kwa kumzawadia dola milioni 1, Juan ingawa kwa sasa wanaangalia video za tukio hilo ili kujua kama masharti yote ya zawadi hiyo yalifuatwa.

Sharti la kushinda kitita hicho kinono lilikuwa ni kujitokeza mbele ya rais Obama na kuhakikisha Obama amekuona na pia kutamka kwa sauti kubwa “Battlecam.com” mara sita.

Ingawa Juan huenda akashinda dola hizo milioni 1, alikamatwa polisi na kufunguliwa mashtka ya kujianika hadharani kinyume cha maadili ya jamii.

No comments:

Post a Comment