KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 2, 2010

Agundua Mumewe Ana Mke Mwingine Kwenye FacebookMwanamke mmoja aliyeolewa hivi karibuni nchini Australia alipigwa na butwaa baada ya kugundua kupitia mtandao wa Facebook kuwa mumewe alikuwa na mke mwingine aliyemuoa wiki moja kabla ya harusi yake.
Kwa mujibu wa gazeti la Fairfax, mwanamke huyo alipigwa na butwaa baada ya kuona picha za harusi ya mumewe na mwanamke mwingine kwenye Facebook.

Gazeti hilo lilisema kuwa mwanamke huyo aliyejulikana kwa kifupi kama Bi Hiu, alimgundua mke mwenza wa mumewe ndani ya mwezi mmoja baada ya kufunga ndoa na Bwana Ling.

Mwanamke huyo ambaye hivi sasa anadai talaka yake, alisema kuwa Ling alisafiri kwenda Hong Kong kwenda kumuoa mpenzi wake wa zamani zikiwa ni wiki chache kabla ya harusi yao.

Naye Bwana Ling aliliambia gazeti la Sunday Morning Herald la Australia kuwa ndoa yake ya Hong Kong iliandaliwa na wazazi wake na yeye alishinikizwa kufuata maagizo ya wazazi wake.

"Aliniambia anaenda China kuitembelea familia yake", Bi Hiu aliiambia mahakama ya masuala ya familia nchini Australia.

Hiu aliiambia mahakama hiyo kuwa mama yake Ling alishtushwa aliposikia Ling ana mke mwingine nchini Australia na alikuwa hajui lolote kuhusiana na ndoa hiyo hadi alipofahamishwa baadae.

Ling anakabiliwa na tuhuma ya ulaghai na kuoa mke zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja bila ya wake zake hao kujua na huenda akatupwa jela miaka mitano

No comments:

Post a Comment