KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, October 12, 2010

Meno zaidi ya 150 yakamatwa na ngozi nane za chui
MENO ya tembo yapatayo 154 na ngozi za chui pamoja na mikia miwili ya tembo, imefanikiwa kukamatwa na jeshi la polisi nchini wakati wakijaribu kutorosha nyara hizo za serikali.
Taarifa hiyo iltolewa jana, na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleman Kova wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Kova alisema kuwa nyara hizo zilikatwa na watuhumiwa tofauti watatu na kila moja alikutwa na nyara hizo akiwa amezibeba kwenye gari.

Alisema mtuhumiwa wa kwanza alikutwa maeneo ya Kimara akiwa amebeba meno ya tembo katika gari lake ambapo alizifunga na kugundulika.

Na wawili walikutwa maeneo ya Kariakoo Msimbazi wakiwa wamebeba ngozi nane za chui wakiwa wamezihifadhi garini

No comments:

Post a Comment