KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, October 2, 2010

Askari wauana kwa wivuASKARI MAGEREZA wa kike Mwajabu Ramadhani (22), mkazi wa Babati, mkoani Manyara, ameuawa kwa kupigwa risasi na askari mwenzake ambaye imedaia ni mpenzi wake wa zamani kwa kile kilichodaiwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Palmera Sumari, alisema tukio hilo, lilitokea Septemba 29, mwaka huu, majira ya saa 3 asubuhi, huko katika kambi ya Magereza mkoani humo

Amesema kuwa, siku ya tukio marehemu alikuwa katika gereza hilo akiangalia wafungwa wa kike kuwasimamia katika shuhguli za kila siku na alitokea askari Wilbrod Gwandu [26] na kummiminia risasi bada ya kushindwa kumjibu majibu sahihi aliyeulizwa na mtuhumiwa huyo.

Ameswema kuwa mara baada ya kumkuta askari huyo akwia na wafungwa hao mtuhumiwa Wilbrod alimuuliza marehemu kuwa ni kwanini alimaua amuache na badae alifyatua risasi iliyopata maeneo kifua na gotini na kufariki dunia papohapo.

Kamanda huyo alisema kuwa, mara baada kumpiga risasi marehemu nay eye alichukua bunduki hiyo kwa lengo la kujifyatulia risasi maeneo ya kichwani na badala hakufanikiwa na badala yale alijijeruhi.

Hata hivyo alidai kuwa askari huyo mtuhumiwa alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, amelazwa anaendelea na matibabu huku akiwa chini ya ulinzi na hali yake inadaiwa inaendelea vizuri na hali yake itakapotengemaa atafikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji

No comments:

Post a Comment