KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 21, 2010

Wimbi la wanawake matapeli laibuka kwa kasi



JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewatahadharisha wananchi wake hasa madereva wa magari kuwa makini katika shughuli zao kutokana na kuzuka wimbi la wanawake matapeli wanaopora magari kwa kuwarubuni.
Tahadhari hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Kova alisema, wanatoa taarifa hii kwa umma ili uweze kutambua kuzuka kwa wimbi la wanawake matapeli waliozagaa jijini na kwingineko na kujipatia na kupora magari kwa njia ya udanganyifu.

Alisema kuwa wanawake huwa wanatumia mavazi la heshima la hijabu na kukodi magari hayo na kuzunguka na dereva huyo kumuamuru apelike watoto shule ama, alitumie kwenye sherehe kama harusi ama shughuli nyingine atakayomuamuru dereva.

Alisema wanawake wengi ambao wameshakamatwa huwa wanatumia kuwawekea madereva hao kilevi kwenye kinywaji anachomnunulia dereva huyo kasha kutoweka na gari biloa mwenyewe kutambua.

Hivyo tahadhari hiyo imetolewa ili madaereva kluwa macho na hasa wamiliki wa magari ili kuweza kupiunguza tatizo hilo ambalo linakuja kwa kasi na jeshi hilo limesema liko aktika msako kuwasaka wanawake wengine wanaoshirikiana katika uporaji huo

No comments:

Post a Comment