KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 21, 2010

Waziri mkuu wa Somalia amejiuzulu baada ya kuwepo mvutano wa madaraka na Rais wa nchi hiyo



Serikali ya Rais Sheikh Sharif Ahmed inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inapambana na kundi la wapiganaji la al-Shabab kudhibiti mji mkuu Mogadishu.



Omar Abdirashid Ali Sharmarke

Waandishi wanasema mabishano na waziri mkuu huyo yamerejesha nyuma mapambano dhidi ya wapiganaji.

Omar Abdirashid Ali Sharmarke amekuwa akishinikizwa kwa miezi kadhaa ili ajiuzulu.

Alisema alishindwa " kufanya kazi na Rais".

Wanamgambo hao kwa sasa wanadhibiti eneo kubwa la Somalia ya kusini na ya kati, na serikali inayoungwa mkono na majeshi ya kutunza amani ya Umoja wa Afrika, inadhibiti maeneo machache kwenye mji mkuu huo.

Bw Sharmarke aliwaambia waandishi kwamba aliamua kujiuzulu "baada ya kuangalia mgogoro wa kisiasa uliopo serikalini na ukosefu wa usalama unavyoongezeka Somalia".

Rais Ahmed amemshukuru kwa "uamuzi wake wa kishujaa".

Viongozi hao wawili wameshindwa kukubaliana juu ya rasimu mpya ya katiba.

Kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu huyo ilikuwa ipigwe mwishoni mwa wiki lakini ikaahirishwa.

Mwezi Mei, Bw Sharmarke alisema kura ya kupigwa bungeni ya kutaka ang'atuke ni kinyume cha sheria

No comments:

Post a Comment