KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 21, 2010

Ni shinikizo la damu kifo cha mkemia mkuu



JESHI la Polisi mkoa wa Tanga, kimetoa taarifa ya awali kuhusiana na uchunguzi wa kifo cha ghafla cha mkemia mkuu wa Serikali Dk. Ernest Mashimba kilichomkuta akiwa nyumba ya wageni wilayani Lushoto na kusema imegundulika kuwa chanzo cha kifo chake
Uchunguzi huo awali uliofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto, na kubaini kuwa alifariki mara baada ya kupata tatizo hilo akwia chumbani kwake.

Taarifa hiyo ilitolewa jana mbele ya waandishi wa habari na Ofisa mwandamizi wa jeshi la Polisi Mkoani Tanga, Bi Adolphina Kapufi.

Kapufi aliendelea kutoa taarifa hiyo kwa kusema kuwa, uchunguzi huo wakati unafanyika ulibaini kuwa marehemu kabla ya kupata BP chumbani kwake walikuta mabaki ya chakula kilicholiwa na mboga ya samaki na pombe aina ya Heinken ambazo walikuta chupa hizo hazijafunguliwa na kabla ya kwenda kulala ilidaiwa marehemu alikunywa bia aina ya Castle akiwa mapokezi.

Hata hivyo Bi Kaputi alisema kuwa jeshi hilo lipo linaendelea na uchunguzi zaidi na yatakayobainika yatajulishwa kwenye vyombo vya habari .

Mashimba alifariki akiwa Lushoto usiku wa kuamkika Jumamosi ambapo alikwenda wilayani humo kwa lengo la kuhudhuria mahafali ya binti yake katika shule ya sekondari Kifungilo

No comments:

Post a Comment