KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 14, 2010

Wazazi wajifunze kutokana na matukio haya



WAZAZI nchini wametakiwa kuwa makini na watoto wakati wa vipindi vya sikukuu kutokana na matukio na vifo vinavyowakumba watoto hao katika sikukuu hizo.
Rai hiyo imetolewa na viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kutokana na tukio lililotokea katika sikuuu ya Idd Pili katika ukumbi wa Luxury Pub Temeke jijini Dar es Salaam.

Watoto wawili waliweza kupoteza maisha katika ukumbi huo baada ya umeme kukatika ghafla katika ukumbi huo na watoto kuanza kukanyagana huku na huko na hatimaye kupatikana idadi hiyo ya vifo na wengine kuwa na hali mbaya ya kiafya baada ya mtafaruku huo.

Watoto hao walipoteza maisha baada ya kukanyagwa na wengine waliweza kuzirai baada ya kukoisa hewa kutokana mlundikano wa watoto waliokuwa wakisherehekea disco toto katika ukumbi huo.

Tukio kama hilo lilitoke amwaka juzi huko mkoani Tabora baada ya ukumbi umeme kuktika na watoto hao kukosa hewa na kupatikana vifo vya watoto kadhaa hali iliyofanya nchi isisimke kutokana na tukio hilo ambalo liligusa watu wengi.

Matukio kama haya wazazi kote nchini walitakiwa wawe makini na watoto wao hasa katika kusherekekea sikukuu zinazowakutanisha watoto wengi katika kumbi.

Hivyo wazazi hao wametakiwa na kukumbushwa kuwa hakuna ulazima wea kuwapeleka weatoto hao katika kumbi hizo na kusababisha vifo vyao na kutakiwa kusherehekea wakiwa katika sehemu tulivu.

Taarifa iliyotolewa jana jioni na wauguzi wa hospitali ya Temeke ambako watoto hao walikimbiziwa hapo kwa ajili ya matibabu ilidaiwa kuwa idadi kubwa ya watoto waliofikishwa hapo watakabiliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu ambako wengi wao wameshagundulika kukabiliwa na tatizo hilo

No comments:

Post a Comment