KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 14, 2010

Mzungu wa Mtibwa Afukuzwa Nchini Kwa Lugha ChafuALIYEKUWA Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa, Greg Swart, amefukuzwa nchini kwa makosa ya lugha zisizovumilika kwa watumishi ikiwemo na kukiuka taratibu na sheria za kazi.
Serikali imemfukuza meneja huyo ambaye ni raia wa Afrika Kusini baada ya malalamiko ya wafanyakazi wa kiwandani hapo kumfikia Rais Kikwete katika ziara yake za kampeni mkoani Morogoro alipotembelea kiwandani hapo.

Swart alikuwa akilalamikiwa na wafanyakazi, viongozi wa Serikali wakiwemo na wakulima kwa kuwa na lugha kali na zaudhalilishaji na kukiuka maadili ya utumishi ambayo ilikuwa kero kwa muda mrefu kwa wafanyakazi kiwandani hapo..


Hivyo kutokana na taarifa iliyosomwa mbele ya Jk iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomelo, Bi Fatma MWasa maazimio yaliyofikiwa ni kuajiria meneja mpya kiwandani hapo na kurekebisha malalamiko yote ya wafanyazi kiwandani hapo

No comments:

Post a Comment